Top ad

Top ad

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017



Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo, DAS wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Gift Msuya wakifatilia dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017

Baadhi ya Wananchi waliozuru katika dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akitoa taarifa ya Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Alhamisi June 1, 2017 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.
Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo  Mhe Paul C. makonda  amesema kuwa jumla ya Miradi 40 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam yenye thamani ya Shilingi 244,392,530,334 huku akibainisha kuwa Miradi 12 imezinduliwa, Miradi 15 imewekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili imefunguliwa na Miradi 11 imetembelewa.
Rc Makonda alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo , uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 wenye kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu pia umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya jitihada ya kudhibiti ni ajenda muhimu kwa mustakabali wa maisha ya mtanzania kwa kuwa linagusa nguvu kazi ya Taifa.
"Katika kutimiza adhma iliyowekwa na waasisi wa Taifa la Tanzania wakati wa kuanzisha Mbio za Mwenge kama kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, uzalendo, Umoja, Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu, mkoa wetu wa Dar es salaam ulipokea Mwenge wa Uhuru siku ya tarehe 25/05/2017 saa 3 asubuhi katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma ukitokea Mkoa wa Lindi na kukabidhiwa katika wilaya ya Temeke ambapo ndipo ulipoanza kukimbizwa" Alisema Mhe Makonda

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam kuanzia Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo  na kuzindua miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Mhe Makonda amewashukuru wakazi wote wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ulipopita.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Pwani Mhe Ernest Ndikilo amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Pwani utazuru katika Wilaya zote Saba zilizopo katika Mkoa huo sambamba na kuzindua, Kutembelea, na kuweka Mawe ya Msingi katika miradi mbalimbali.
Alisema Miradi hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni themanini na tano.
Mhe Ndikilo alisema kuwa Mkoa wa Pwani una maendeo makubwa na ya kutosha katika uwekezaji hususani uwekezaji wa Viwanda hivyo amewasihi wananchi kwa umoja wao Kwenda  kuwekeza Mkoani Pwani
Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali. Hii ilitokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya nchi  kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Hongera Dar es salaam !!!

habari kwa hisani ya : http://wazo-huru.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment

 
Top