Top ad

Top ad




Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuonesha juhudi, kuwa na uchu wa maendeleo, dhana ya kujiajiri pamoja na kiu ya kugundua na kujishirikisha katika ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kimaisha.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kazi ajira vijana na walemavu Mh. Jenista Mhagama, katika sherehe za ufunguzi wa wiki ya vijana zinazofanyika Mkoani Simiyu, katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Amesema vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wawezeshwe ili waweze kutambua umuhimu walionao katika kulijenga Taifa la Tanzania.
Maadhimisho haya ya wiki ya vijana yanaambatana na kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru isemayo ”vijana ni nguvukazi ya Taifa washirikishwe na kuwezeshwa” ambapo kilele chake ni tarehe 14/10/2016.(Habari na Martha Kawishe- Manispaa ya Kinondoni)

0 comments:

Post a Comment

 
Top