TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA DMDP NA TARURA KINONDONI. Posted On: June 21st, 2019 Hayo yamethibitika leo wakati Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwa lengo la kujiridhisha na ubora wake ikiwa ni pamoja na kuangalia hatua za utekelezaji zilizofikwa. Amesema utekelezaji wa miradi hii kwa mkoa wa Dar es salaam ni ya muhimu sana kwani itatatua kero kubwa walizokuwa wakizipata wananchi hasa yale maeneo waliyokuwa wakisumbuliwa na mafuriko na zile zilizokuwa na uharibifu mkubwa. "Miradi hii ni muhimu sana kwani inaenda kubadilisha sura ya Dar es salaam, tunachotaka kama Serikali ni kuhakikisha kero kwa wananchi zinaondolewa na hata wale walioko masomoni wakirudi, tuwashike mikono, taswira ibadilike "Amesisitiza Jafo. Naye Mratibu wa DMDP Manispaa ya Kinondoni Ndg. Mkelewe Tungaraza alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya DMDP amesema dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaisimamia na kuitekeleza kwa kiwango kinachotakiwa ili ilete tija kwa wananchi husika. Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amewataka wananchi kuhakikisha wanazitunza na kuzifanyia usafi barabara hizo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kutupa taka kwenye mitaro kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri ubora na Mazingira kwa ujumla. Kadhalika amewataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha suala la uwekaji wa alama za barabara hizo,, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa weledi, kwa kuzingatia vigezo na viwango vya ubora ili miundombinu hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu huku ikiendelea kusaidia wananchi. Katika ziara hiyo aliyotembelea barabara ya Mbezi Makonde, Kilongawima, akachube na makanya pia imehudhuriwa na wakuu wa wilaya ya Ubungo na Kinondoni, wakurugenzi, wakandarasi pamoja na waratibu wa TARURA na DMDP. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA DMDP NA TARURA KINONDONI. Posted On: June 21st, 2019 Hayo yamethibitika leo wakati Waz... + Read more »
KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA, KINONDONI YAADHIMISHA KWA VITENDO Posted On: June 14th, 2019 Kuelekea siku ya kilele cha Mtoto wa Afrika chenye kauli mbiu isemayo "Mtoto ni msingi wa Taifa endelevu tumutunze, tumlinde na kumuendeleza", Kinondoni yaadhimisha kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji maalumu pamoja na michezo. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika sherehe hizo zilizofanyika Kiwilaya katika shule ya msingi Magomeni, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi. Stella Msofe amesema watoto ni hazina ya Taifa, hivyo wanapaswa kulindwa, kutunzwa, kuthaminiwa, kuheshimiwa na kubwa zaidi kuwapatia haki za msingi kama elimu na afya. Ameongeza kuwa wakati umefika wa Serikali kutofumbia macho unyanyapaa wa watoto wenye mahitaji maalumu hususani ulemavu wa viungo vya mwili kwani wanayo haki na nafasi sawa katika jamii, hivyo wapewe nafasi wanayostahili na kupatiwa vipaumbele kama watoto kwani ndio warithi wa baadae wa Taifa hili. "Leo hii Tanzania tunajivunia maendeleo yanayosimamiwa na Mh Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, naye aliwahi kuwa mtoto akakuwa, akatunzwa akapewa haki zake, na leo hii ndiye kiongozi shupavu, yote hii ni kwasabababu aliandaliwa vema mpaka amekuwa na uwezo huo na sisi kama jamii tukitenda haki sawa kwa kuwathamini wote bila kujali hali zao, tutakuwa tunaandaa viongozi bora wa baadae" amesisitiza Bi Stella. Naye Bi. Halima Kahema ambaye ni Mkuu wa Idara ya idara ya maendeleo ya jamii katika Manispaa hiyo akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi amesema Manispaa yake iko tayari kushirikiana na Asas hizi katika kuhakikisha haki ya mtoto inatekelezwa na wahitaji wananufaika nayo. Katika maadhimisho hayo yaliyoambatana na utoaji wa vyeti vya ushiriki za Asas sita, pamoja na zawadi za madaftari na fulana kwa watoto, pia yalipambwa na michezo ya kukimbia, kuruka kamba na kukimbiza kuku . Asas zilizoshiriki katika maadhimisho hayo ni Kihowede, AHRN, Save the children, PDF (peopale development forum), Red cross na Tiba. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA, KINONDONI YAADHIMISHA KWA VITENDO Posted On: June 14th, 2019 Kuelekea siku ya kilele cha M... + Read more »
KINONDONI YASAINI MIKATABA NA MAKAMPUNI MAWILI YA TAKRIBANI BILIONI 58 Posted On: June 13th, 2019 NI KWA AJILI YA UJENZI NA MABORESHO YA MTO NG'OMBE NA BARABARA YA SHEKILANGO KWA KIWANGO CHA NJIA NNE. Akisaini mikataba hiyo, kati yake na makampuni hayo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg. Aron Kagurumjuli amesema, mradi wa mto ng'ombe utakaogharimu bilioni 32, utajengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group CO. LTD na mradi wa barabara ya shekilango wa njia nne utakaogharimu shilingi 26 bilioni, utajengwa na Kampuni ya China road and bridge Cooperation hali itakayosaidia si tu kuboresha maeneo hayo bali pia kuyapandisha hadhi kwa kiwango kusudiwa. Amesema katika mikataba hiyo pia yatajengwa mabwawa ya kukusanyia maji eneo la karibu na chuo cha maji kutoka maeneo mbalimbali na maji hayo yataruhusiwa kuingia taratibu mto ng'ombe hali ambayo itasaidia kupunguza mafuriko. Akishuhudia utilianaji sahihi mikataba hiyo, Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta amesema, Serikali ya awamu ya tano ni Serikali sikivu yenye lengo la kuboresha makazi duni na kuwatoa wananchi kwenye kifungo cha mateso ya mafuriko, na ujenzi huu wa mto ng'ombe utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kadhia hiyo iliyokuwa ikisumbua wananchi wa maeneo ya Tandale na kijitonyama. Aidha Meya Sitta pia amewataka makandarasi wanaojenga miradi hiyo kujenga kwa wakati na kwa ubora stahiki ili waweze kumaliza kero iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YASAINI MIKATABA NA MAKAMPUNI MAWILI YA TAKRIBANI BILIONI 58 Posted On: June 13th, 2019 NI KWA AJILI YA UJENZI NA MABORESHO Y... + Read more »
ELIMU YA AFYA, UZAZI NA UPIMAJI NA USHAURI NASAHA KWA WANANCHI YATOLEWA KINONDONI. Posted On: June 7th, 2019 Kinondoni kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la JHPIEGO lenye kauli mbiu ya "TUPANGE PAMOJA"yaendesha zoezi la utoaji elimu ya Afya ya Uzazi, upimaji na ushauri nasaha kwa wananchi ili kulinda na kuboresha afya zao. Akifafanua kuhusu zoezi hilo, lililofanyika katika mtaa wa Hananasif Kinondoni, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr Festo Ndugange amesema kuwa kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano ni kujenga na kukuza uchumi wa nchi kupitia Viwanda, katika kuhakikisha hilo linatimia wanahitajika watu wenye afya njema kimwili na kiakili ili waweze kutoa mchango utakiwao kwa wakati sahihi. "Wakati viongozi wetu wanapigania masuala ya kukuza uchumi wanahitaji mwitikio chanya kutoka kwenye jamii na hilo linawezekana endapo jamii hiyo itakuwa na watu wenye afya njema na nguvu imara, nasi tumeona namna nzuri ya kutoa mchango wetu ni kuwapa elimu, kinga na tiba imara wakati wote" ameongeza Dr Festo. Akiongea katika zoezi hilo, mratibu wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto Manispaa ya Kinondoni Bi. Edith Manase Mboga amesema, huduma na elimu inayotolewa inalenga kupunguza au kumaliza kabisa matatizo yanayoikumba jamii hasa ikizingatiwa chanzo chake ni ukosefu wa uelewa na kutokuwa na uthubutu wa familia kukaa na kuweka mikakati ya pamoja juu ya masuala ya afya. Huduma walizopatiwa wananchi hao ni elimu juu ya afya ya uzazi, upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti, shinikizo la damu, ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU. Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wameishukuru Manispaa ya Kinondoni kwa fursa hiyo adimu itakayowawezesha kupata elimu juu ya mwasuala ya Afya ya uzazi pamoja na athari azipatazo mtu asiyefuata masuala hayo ya Afya. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. ELIMU YA AFYA, UZAZI NA UPIMAJI NA USHAURI NASAHA KWA WANANCHI YATOLEWA KINONDONI. Posted On: June 7th, 2019 Kinondoni kwa kushirikiana... + Read more »
ELIMU YA AFYA, UZAZI NA UPIMAJI NA USHAURI NASAHA KWA WANANCHI YATOLEWA KINONDONI. Posted On: June 7th, 2019 Kinondoni kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la JHPIEGO lenye kauli mbiu ya "TUPANGE PAMOJA"yaendesha zoezi la utoaji elimu ya Afya ya Uzazi, upimaji na ushauri nasaha kwa wananchi ili kulinda na kuboresha afya zao. Akifafanua kuhusu zoezi hilo, lililofanyika katika mtaa wa Hananasif Kinondoni, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr Festo Ndugange amesema kuwa kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano ni kujenga na kukuza uchumi wa nchi kupitia Viwanda, katika kuhakikisha hilo linatimia wanahitajika watu wenye afya njema kimwili na kiakili ili waweze kutoa mchango utakiwao kwa wakati sahihi. "Wakati viongozi wetu wanapigania masuala ya kukuza uchumi wanahitaji mwitikio chanya kutoka kwenye jamii na hilo linawezekana endapo jamii hiyo itakuwa na watu wenye afya njema na nguvu imara, nasi tumeona namna nzuri ya kutoa mchango wetu ni kuwapa elimu, kinga na tiba imara wakati wote" ameongeza Dr Festo. Akiongea katika zoezi hilo, mratibu wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto Manispaa ya Kinondoni Bi. Edith Manase Mboga amesema, huduma na elimu inayotolewa inalenga kupunguza au kumaliza kabisa matatizo yanayoikumba jamii hasa ikizingatiwa chanzo chake ni ukosefu wa uelewa na kutokuwa na uthubutu wa familia kukaa na kuweka mikakati ya pamoja juu ya masuala ya afya. Huduma walizopatiwa wananchi hao ni elimu juu ya afya ya uzazi, upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti, shinikizo la damu, ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU. Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wameishukuru Manispaa ya Kinondoni kwa fursa hiyo adimu itakayowawezesha kupata elimu juu ya mwasuala ya Afya ya uzazi pamoja na athari azipatazo mtu asiyefuata masuala hayo ya Afya. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. ELIMU YA AFYA, UZAZI NA UPIMAJI NA USHAURI NASAHA KWA WANANCHI YATOLEWA KINONDONI. Posted On: June 7th, 2019 Kinondoni kwa kushirikiana... + Read more »
WADAU NA JAMII KWA UJUMLA WAMETAKIWA KUONESHA UPENDO KWA KUWAKUMBUKA NA KUWAJALI WATU WENYE UHITAJI MAALUMU KATIKA JAMII. Posted On: May 31st, 2019 Hayo yamebainika leo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo kwa kushirikiana na asas ya Human releif foundation walipozuru katika kituo cha watoto yatima cha Kijiji cha Furaha kilichopo Mbweni na kutoa msaada wa sukari, unga, mafuta ya kupikia na mchele kwa kituo hicho. Amesema ni jukumu letu kuhakikisha watoto hawa wanapatiwa upendo unaostahili ikiwemo haki za kisheria za watoto ambazo ni kulindwa, kusikilizwa, kupatiwa elimu, makazi na malazi. Amesema "Watoto hawa ni jukumu letu sote, lazima tuwapende na kuwajali, kwani jamii yetu imezungukwa na watu mbalimbali wanaohitaji kutazamwa kwa jicho la tatu kama vile watoto yatima na wengineo, hivyo ni wajibu wetu kuwapatia vitu wanavyohitaji".Mhe. Chongolo Ameongeza kuwa kilichofanywa leo na Mr Mbarak F.Baghumesh kutoka asas ya Human Releif Foundation ni ishara kubwa ya upendo na inatakiwa kuigwa na kila mtu, kwani hata yeye hajaangalia dini yake isipokuwa ametanguliza upendo na uthamani wa kiutu. Aidha ameahidi kushirikiana bega kwa bega na wadau wengine katika kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazoikabiri taasisi ya Kijji cha Furaha zinatatuliwa na kuwataka watu wa idara ya ustawi wa jamii Manispaa ya Kinondoni kutafuta njia mbadala za kuwasaidia watoto yatima wanaomaliza shule katika vituo mbalimbali. Kwa upande wake Mr Mbarak ambaye ni Operation Manager wa shirika la Human Relief Foundation, amesema kuwa mbali na kutoa msaada hui, ataendelea kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kuwathamini watu wenye mahitaji maalum bila kujali rangi wala dini zao. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WADAU NA JAMII KWA UJUMLA WAMETAKIWA KUONESHA UPENDO KWA KUWAKUMBUKA NA KUWAJALI WATU WENYE UHITAJI MAALUMU KATIKA JAMII. Posted On: May ... + Read more »
DC KINONDONI AKEMEA VIKALI WAKANDARASI WAZEMBE Posted On: May 31st, 2019 NI WALE WASIOFANYA KAZI ZAO KWA WELEDI, HALI INAYOPELEKEA UCHELEWESHWAJI WA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO. Kauli hiyo imetolewa leo, na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo katika ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kujiridhisha na hatua za utekelezaji zilizofikiwa. Amesema wakandarasi ni lazima waelewe umuhimu wa kutekeleza na kukamilisha miradi hii kwa mujibu wa makubaliano na mikataba waliyoingia kwani kwa kutokufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo na ni kutoitendea haki si tu Serikali bali hata wananchi walengwa wa mradi unaotekelezwa. Aidha Mhe. Chongolo ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya CRJE East Africa LTD kwani katika kipindi Cha miezi 11 ya mkataba wake mradi huo umekamilika kwa asilimia 20 pekee na huku akiwa amebakiwa na miezi 7 ya kumaliza mkataba. Amesema "wakandarasi Kama hao hawatavumiliwa katika Wilaya yangu na endapo itafika tarehe 30 mwezi June bila kuonesha dalili za mabadiliko ya mradi huo mkandarasi huyu achukuliwe hatua sitahiki.", Mh. Chongolo. Kadhalika amekemea tabia ya baadhi ya wakandarasi wakubwa kuchukua tenda za Ujenzi na baadae kuwapa kandarasi wengine au wadogo kuifanya kazi hiyo, huku wao wakibaki kuwa kama madalali. Katika hatua nyingine amewataka watendaji wa Kata kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na iweze kuleta tija kwa jamii Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa wilaya leo ni pamoja na Barabara ya Tegeta nyuki, Barabara ya Boko Magereza, Hospitali ya Wilaya ya Mabwepande, Shule ya wasichana ya Mabwe Tumaini girls, Kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande na Shule ya wavulana ya Mbweni Teta. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. DC KINONDONI AKEMEA VIKALI WAKANDARASI WAZEMBE Posted On: May 31st, 2019 NI WALE WASIOFANYA KAZI ZAO KWA WELEDI, HALI INAYOPELEKEA UCHE... + Read more »