Top ad

Top ad

KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI MANISPAA YA KINONDONI, YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Posted On: August 28th, 2018
Ziara hiyo iliyoongozwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh George Mangalu Manyama ambae pia ni Diwani wa Kata ya kigogo imepata fursa ya kukagua utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo ikiwa ni kwa lengo la kujiridhisha  ubora unaoenda sambamba na ukamilishwaji wake ikihusisha hatua za ukamilishaji pamoja na thamani ya fedha iliyotumika.
Katika ziara hiyo iliyohusisha wajumbe wa Kamati hiyo ya fedha ambao ni Wah. Madiwani,   wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalam imetembelea na kukagua  mradi wa ujenzi wa madarasa manne shule ya msingi Mivumoni, ujenzi wa barabara ya Makanya iliyoko Tandale, ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua barabara ya Ntuze iliyoko Kinondoni, pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Mikoroshini iliyoko Kata ya Msasani.
Mh Mangalu amesema hatua iliyofikiwa miradi hii ni nzuri na ya kuridhisha, inayoonesha mwelekeo wa dhamira ya dhati  ya utekelezaji na ukamilishaji  wa miradi ya maendeleo itakayotoa huduma bora kwa Wananchi.
"Miradi hii ni mizuri, na inaridhisha, tuhakikishe inamalizwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma bora katika jamii" Amesema Mh.Mangalu.
 Aidha amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanaitunza na kuithamini miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao, ikiwa ni pamoja na kuwa walinzi wa uchafuzi wa mazingira na   kuhakikisha wanaitunza mitaro ili iweze kutumika kwa makusudi kamili.

Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top